Jumatatu 11 Mei 2026 - 11:00
Wananchi wa Ireland hawataki ushirikiano na utawala unaotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari

Hawza/ Kundi la wafuasi wa michezo nchini Ireland limetuma barua ya wazi kwa Shirikisho la Soka la Ireland (FAI) na kuutuhumu utawala wa Israel kwa kufanya “mauaji ya kimbari” wakati wa vita vya Ghaza. Pia wametangaza kwamba Ireland, iwapo itakubali kufanyika kwa mechi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, itakuwa imekiuka sheria za UEFA na FIFA.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kundi la mashabiki lilituma barua yenye anuani isemayo “Simamisheni Mchezo” kwa shirikisho hilo, ambayo ilisainiwa na wachezaji wa Ligi ya Ireland. Miongoni mwa waliotia saini ni Brian Kerr, kocha wa zamani wa timu ya taifa, na Louise Quinn, mchezaji wa zamani na mshindi mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa wanawake.

Roberto Lopez, Rais wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa wa Soka Ireland alisema: “Hatuwezi kupuuza janga la kibinadamu nchini Palestina; kupotea kwa maisha ya watu huko Ghaza kunapaswa kutangulia mbele ya aina yoyote ya masuala ya kimichezo.” Pia walitangaza kwamba Ireland, iwapo itakubali kufanyika kwa mechi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, itakuwa imekiuka sheria za UEFA na FIFA.

Chanzo: Dearborn

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha